Hopes Never Die.
Matumaini HAYAFI Kamwe.
IBADA NA SALA:
Tenga Muda UKASALI.....Ni hilo Jambo lenye Uwezo Mkuu Duniani.
UNAPOSALI........
"Sema UNACHOKUSUDIA, na KUSUDIA unachosema."
"Sali bila kukoma."
"Mungu anaongoza ULIMWENGU, lakini Sala Zinamwongoza MUNGU."
Sala ndiyo SILAHA bora tuliyo nàyo; ni ufunguo wa moyo wa Mungu. Ni lazima uongee na Yesu si kwa mdomo tu, bali kwa moyo wako. Kwa kweli katika matukio fulani, unapaswa kuzungumza naye tuū kwa moyo wako..... "Mt. Padre PIO."
KATIKA SALA;
1.) Kuwa na Moyo MNYENYEKEVU.
2.) Omba kwa Bwana kwa UAMINIFU.
3.) Omba ili mapenzi ya Mungu yatimizwe.
4.) Omba kwa Bwana kwa ustahimilivu na azimio na usikate tamaa.
5.) Omba kwa IMANI thabiti.
EWE MWANADAMU:
1.) Tenga mudà wa kusoma maandiko ya siku pamoja na ufafanuzi. Jipe mudà wa kufanya tafakari na Sala. Hivyo sikiliza kwa moyo, utagundua na kuuelewa ujumbe wa Mungu.
2.) Ufanye ujumbe huo kuwa wako kiasi cha hata kuwa huru kuandika jambo juu ya ujumbe huo bila kuacha kitu.
3.) Andika hisia zako zote ulizozipata kwa siku nzima: hisia za upendo, hofu, hatia au hasira. Andika mawazo yako na utakavyoyatimiza, maazimio yako, mazungumzo katika nafsi yako, ndoto zako, matarajio na mategemeo yako, mwitikio wako katika matukio na kwa watu.
4.) Kuwa mbunifu na tunga Sala zako, mashairi, methali na tenzi.
5.) Utakapoangalia nyuma na kusoma vyote, utaanza kuona na kujigundua zaidi kuhusu wewe mwenyewe. Kisha itakuwa tuu sio tu mazungumzo ndani ya nafsi yako bali na Mungu ambaye daima anaongea na yupo kupitia neno lake.
AMINA!
if the data has not been changed, no new rows will appear.
Day | Followers | Gain | % Gain |
---|---|---|---|
August 26, 2023 | 559 | +98 | +21.3% |
September 30, 2022 | 461 | +17 | +3.9% |
August 09, 2022 | 444 | +28 | +6.8% |
July 03, 2022 | 416 | +37 | +9.8% |
May 27, 2022 | 379 | +49 | +14.9% |
April 19, 2022 | 330 | +52 | +18.8% |
March 12, 2022 | 278 | +25 | +9.9% |
January 13, 2022 | 253 | +4 | +1.7% |
December 07, 2021 | 249 | +8 | +3.4% |