NGOME KATOLIKI on Clubhouse

NGOME KATOLIKI Clubhouse
4.8k Members
Updated: Feb 2, 2024

Description

JUMUIYA YA MTAKATIFU PAPA YOHANE PAULO II MTANDAONI

JUMUIYA YA SALA YA KIKATOLIKI TANGU JULY 27 2021📍🗓

✝️

RATIBA YA SALA ZA JUMUIYA

🙏 Rozari ya Huruma ya Mungu - Saa 08:50 Usiku (02:50 am)

🙏 Rozari ya Moyo Mtakatifu wa Yesu - Kila Siku Saa 11:10 Alfjiri (05:10 am)

🙏Sala ya Malaika wa Bwana - Saa 11:55 Asubuhi(05:55am), Saa 05:55 Asubuhi(11:55am) na Saa 11:55 Jioni(17:55pm)

🙏Sala za Asubuhi - Kila Siku saa 12:00 Asubuhi (06:00am)

🙏Rozari ya Huruma ya Mungu - Kila Siku Saa 08:45 Mchana( 14:45pm).

🙏Rozari Takatifu ya Fatima | Tafakari ya Injili | Maisha ya Watakatifu - Kila Siku Saa 02:20 Usiku (20:20pm)

🙏Ibada ya njia ya Msalaba - Kila Ijumaa Saa 08:45 Mchana ( 14:45pm)

🙏Rozari ya Mateso 7 ya Bikira Maria - Kila Jumanne Saa 02:20 Usiku (20:20pm)

✝️

SALA KWA MTAKATIFU YOHANE PAULO WA II

Ee, Mtakatifu Yohane Paulo, kutoka kwenye dirisha la mbinguni, utujalie baraka yako! Libariki Kanisa ulilolipenda na kulitumikia na kuliongoza, ukiliongoza kwa ujasiri katika njia za ulimwengu ili kumleta Yesu kwa kila mtu na kila mtu kwa Yesu. Wabariki vijana, ambao walikuwa shauku yako kubwa. Wasaidie kuota tena, wasaidie kutazama juu tena ili kupata nuru inayoangazia njia ya maisha hapa duniani.

Ubariki kila familia! Ulionya kuhusu shambulio la Shetani dhidi ya cheche hii ya kimungu yenye thamani na ya lazima ambayo Mungu aliwasha duniani. Mtakatifu Yohane Paulo, kwa maombi yako, ulinde familia na kila maisha yanayochanua kutoka kwenye familia.

Ombea ulimwengu wote, ambao bado unatawaliwa na mivutano, vita na ukosefu wa haki. Ulipambana na vita kwa kukaribisha mazungumzo na kupanda mbegu za upendo: utuombee ili tuwe wapandaji wa amani bila kuchoka.

Ee Mtakatifu Yohane Paulo, kutoka kwenye dirisha la mbinguni, tunapokuona karibu na Mariamu, tuma baraka za Mungu juu yetu sote. Amina.
Karibu Sana: Tumsifu Yesu Kristo(Milele Amina). Tupo hapa kwa ajili ya kusali na kuimarishana kiroho. Jambo lolote lisilo endana na Mafundisho ya Ukatoliki halitavumiliwa.

Tuheshimu kila mtu katika Club: Kila mmoja ana nafasi sawa na mwengine! Hatavumiliwa mtu kwa njia yoyote ile ambayo ataonyesha kuvunja heshima na utu wa mwengine. Lugha za matusi haziruhusiwi.

Rules

Karibu Sana

Tumsifu Yesu Kristo(Milele Amina). Tupo hapa kwa ajili ya kusali na kuimarishana kiroho. Jambo lolote lisilo husu Ukatoliki halitavumiliwa.

Tuheshimu kila mtu katika Club

Kila mmoja ana nafasi sawa na mwengine! Hatavumiliwa mtu kwa njia yoyote ile ambayo ataonyesha kuvunja heshima na utu wa mwengine. Lugha za matusi haziruhusiwi.

Last 30 Records

Day Members Gain % Gain
February 02, 2024 4,835 +29 +0.7%
December 19, 2023 4,806 +37 +0.8%
November 08, 2023 4,769 +22 +0.5%
October 09, 2023 4,747 +61 +1.4%
September 09, 2023 4,686 +46 +1.0%
August 11, 2023 4,640 +104 +2.3%
July 10, 2023 4,536 +44 +1.0%
June 17, 2023 4,492 +313 +7.5%
March 16, 2023 4,179 +79 +2.0%
January 12, 2023 4,100 +100 +2.5%
December 01, 2022 4,000 +100 +2.6%
November 05, 2022 3,900 +100 +2.7%
October 10, 2022 3,800 +100 +2.8%
September 12, 2022 3,700 +100 +2.8%
August 27, 2022 3,600 +100 +2.9%
July 25, 2022 3,500 +100 +3.0%
July 06, 2022 3,400 +100 +3.1%
June 16, 2022 3,300 +100 +3.2%
June 09, 2022 3,200 +100 +3.3%
May 07, 2022 3,100 +100 +3.4%
April 23, 2022 3,000 +100 +3.5%
April 09, 2022 2,900 +100 +3.6%
April 03, 2022 2,800 +100 +3.8%
March 18, 2022 2,700 +100 +3.9%
March 11, 2022 2,600 +614 +31.0%
November 23, 2021 1,986 +5 +0.3%
November 22, 2021 1,981 +15 +0.8%
November 19, 2021 1,966 +25 +1.3%
November 16, 2021 1,941 +3 +0.2%
November 15, 2021 1,938 +7 +0.4%

Charts

Some Club Members

More Clubs