RASIMU YA SHERIA YA JUKWAA LA CHEMBA YETU
A. WAHUSIKA (WAJUMBE)
1. Mzaliwa wa chemba (awe anaishi chemba au nje ya chemba)
2. Mkazi wa chemba Kwa kuishi au shughuli za kikazi au biashara
3. Mtu mwingine yeyote anayetaka kujifunza, kuchangia na kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya chemba
B. LUGHA ZITAKAZOTUMIKA
1. Kiswahili
2. Kiingereza
C. MIJADALA
Kutakuwa na mijadala inayohusu masuala ya kiuchumi, kisiasa na kijamii katika ngazi ya;-
1. Kijiji
2. Kata
3. Wilaya
4. Mkoa
5. Kitaifa
6. Kimataifa
NB: 1,2&3 ndio kipaombele zaidi
D. WAJIBU WA KILA MWANAJUKWAA
1. Kukemea uvunjaji wa sheria za jukwaa na zile za serikali pamoja na kanuni kama zitakavyoelekeza.
2. Kujadiliana mada zote atakazokuwa na ufahamu nazo kwa kadri nafasi yake itakavyomruhusu
3. Kuwa mkweli wa taarifa atakazokuwa anazitoa
4. Kulinda haki ya usiri ya Kila mmoja kwenye jukwaa hili
5. Kupendekeza maboresho ya sheria na kanuni za jukwaa kwa kufuata miongozo
6. Kuanzisha mijadala na kuisimamia kama miongozo ya uanzishaji na usimamizi wa mijadala unavyoelekeza
7. Kuheshimu maoni na mawazo ya Kila mwanajukwaa
8. Kutoa elimu, kuhamasisha na kuunga mkono hoja yenye nguvu na itakayokubaliwa na wengi zaidi.
9. Kutoa taarifa Kwa uongozi pale unapotendewa ukatili wa kimtandao au anapotendewa mwenzio.
10. Kujadiliana na kila mmoja kwenye jukwaa hili Kwa heshima na nidhamu na lugha ya staha.
E. MWIKO/MARUFUKU
1. Mijadala ya kikabila, kidini, kikanda na siasa zenye mvutano wa uchama badala ya hoja.
2. Lugha za matusi na zenye kutweza utu wa mtu.
3. Kuanzisha MJADALA katikati ya MJADALA mwingine
4. Kutuma taarifa za uongo au zisizothibitishwa na mamlaka husika.
5. Kutoa taarifa zinazojadiliwa kwenye jukwaa hili na kuzipeleka mahali pengine
6. kutoa taarifa binafsi za wajumbe waliopo humu bila idhini yao ikiwepo mawasiliano Yao ya simu.
7. Kumfuata mjumbe inbox kujadiliana mambo yaliyoko kwenye jukwaa.
8. kulazimisha kuungwa mkono kwenye hoja yako.
WAHUSIKA: 1. Mzaliwa wa chemba (awe anaishi chemba au nje ya chemba)
2. Mkazi wa chemba Kwa kuishi au shughuli za kikazi au biashara
3. Mtu mwingine yeyote anayetaka kujifunza, kuchangia na kusukuma maendeleo
LUGHA: 1. Kiswahili
2. Kiingereza
MIDAJALA: Kutakuwa na mijadala inayohusu masuala ya kiuchumi, kisiasa na kijamii katika ngazi ya;-
1. Kijiji
2. Kata
3. Wilaya
4. Mkoa
5. Kitaifa
6. Kimataifa