WANAZUONI |NA| WASOMI on Clubhouse

WANAZUONI |NA| WASOMI Clubhouse
143 Members
Updated: May 6, 2024

Description

TOFAUTI KATI YA MWAZUONI NA MSOMI✍🏻

Tatu, mwanazuoni huamini kwamba ukweli haugawanyiki, the truth is the whole. Maana yake ni kwamba huwezi kupata ukweli wa jambo kama hujaliangalia jambo hilo katika muktadha wake. Nikitoa ule mfano maarufu, huwezi ukasema kwamba tembo ni kama kamba nene kwa sababu umegusa mkia wake au kwamba tembo ni mpana kwa sababu umegusa sikio lake. Ili kujua ukweli wa umbo la tembo ni lazima uangalie umbo lake zima.


Nitoe mfano mwingine. Ukitaka kuchambua muundo wa kiti, huwezi ukachambua miguu yake tu. Wala huwezi kusema kwamba sehemu za kiti ni miguu na sehemu za kukalia na kuegemea. Ukijumlisha sehemu hizo hutapata kiti, utakachopata ni rundo la mbao! Ukitaka kuelewa muundo wa kiti kizima, huna budi uchambue jinsi, na katika uhusiano upi, sehemu zake zote zimeunganishwa.


Nne, mwanazuoni ni wakala wa mabadiliko ya hali iliyopo, na siyo mtumwa wake. Dhamira yake ni kuigeuza na siyo kuigandisha hali iliyopo. Dhamira yake ni kuleta hali bora katika jamii, hususan kwa walio wengi. Yeye daima ni mpambanaji. Anapambana dhidi ya dhuluma, uonevu, ukandamizaji na uovu mwingine popote pale ulipo. Ndiyo dhamira yake, ndiyo maisha yake, ndiyo uhai wake. Anajitambulisha na wapambanaji wenzake bila kujali wanakotoka, makabila yao, au rangi yao.


Jamaa mmoja alimwandikia Che Guevara kwamba kutokana na majina yao kufanana labda wao ni ndugu wa damu. Che alimjibu kwamba yeye haoni kwamba wao ni ndugu: ‘Lakini’, namnukuu, ‘kama wewe unachukia uonevu popote pale ulipo, basi sisi ni ndugu, makamaradi’ …. bila kujali kama sisi ni ndugu wa damu.
Tano, mwanazuoni hujali, na kupigania maendeleo ya wanadamu, maendeleo ya wote, siyo ya wachache.


Sita, ili kukidhi uelewa wa jamii na mazingira yake na ya ulimwengu, mwanazuoni hujikita kwenye uchambuzi wa kina, uchambuzi ambao unaongozwa na nadharia iliyopevuka. Ndiyo maana wanazuoni wengi, hususan wa Afrika, wanavutiwa zaidi na nadharia ya kimapinduzi ya usoshalisti. Kwa mwanazuoni huyo, ufahamu/elimu ni zana ya kukosoa hali ilivyo bila kusita na kuielekeza kwenye kubadili jamii, siyo bidhaa ya kuuzwa. Katika kusisitiza umuhimu wa nadharia ya kimapinduzi Amilcar Cabral, mkombozi na kiongozi wa Guinea Bissau, alisema: Bila nadharia ya kimapinduzi hakuna mapinduzi yatakayoshinda.

Fully Bofya hapa👇🏻>>
www.chechezaafrika.com

Last 30 Records

Day Members Gain % Gain
May 06, 2024 143 +7 +5.2%
February 18, 2024 136 +2 +1.5%
January 04, 2024 134 +5 +3.9%
November 21, 2023 129 +4 +3.2%
October 19, 2023 125 +3 +2.5%
September 19, 2023 122 +2 +1.7%
August 21, 2023 120 +2 +1.7%

Charts

Some Club Members

More Clubs