kwa miaka mingi, umuhimu wa kilimo endelevu katika kuondoa njaa na umaskini umekuwa mjadala kuntu ulioleta ubishani, ukinzani wa hoja na uliochagizwa. Kwa siku za hivi karibuni, ukweli kuwa;kilimo endelevu ni kitovu cha malengo ya maendeleo hapa Tanzania na kimataifa haukwepeki tena.
Njia za kufikia ukweli huo zinabishaniwa, na mijadala juu ya sera sahihi, teknolojia na uwekezaji .
Ni kwa muono huu, Malembo Farm(MF) inakuletea progamu ya mjadala kuhusu masuala haya hapa nchini na kwingineko duniani uitwao “MF; KILIMO TALK”,utakaokuwa ukiletwa kwako kila siku za wiki kuanzia saa kumi na Moja jioni. 5:00pm EAT
Katika mijadala ya kilimo hivi sasa juu ya maendeleo; mambo makuu sita yanaibuka katika mijadala hiyo. *MF Kilimo Talk* tunayaweka katika mafungu yafuatayo.
1. Biashara, ruzuku na kilimo.
2. Uanzishwaji wa GMO,s
3. Umuhimu wa masoko na kilimo biashara.
4. Umuhimu wa kujitegemea kwa chakula( "Uhuru wa chakula") na ikolojia ya kilimo.
5. Uwekezaji wa sekta binafsi na kutwaliwa kwa rasilimali.
6. Mabadiliko ya tabia nchi.
Kwa nafasi ya kipekee kabisa tunamulika nafasi ya Vijana, Wanawake na Wastaafu Watarajiwa katika masuala haya nyeti.
MF; Kilimo Talk inalenga kuibua mijadala kuhusu mambo haya muhimu na mengine kwa faida ya nchi yetu.
#TafakuriJadidiKwaMstakabaliWaTaifaLetu
Day | Members | Gain | % Gain |
---|---|---|---|
June 19, 2024 | 808 | +5 | +0.7% |
March 17, 2024 | 803 | 0 | 0.0% |
January 26, 2024 | 803 | +2 | +0.3% |
December 13, 2023 | 801 | +1 | +0.2% |
November 03, 2023 | 800 | -1 | -0.2% |
October 04, 2023 | 801 | +3 | +0.4% |
September 04, 2023 | 798 | +3 | +0.4% |
August 07, 2023 | 795 | +4 | +0.6% |