🇹🇿
SHUJAA WA MAENDELEO NA USTAWI WA JAMII TANZANIA (SMAUJATA)*
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum inatarajia kufanya Kampeni ya Kitaifa Kwa Kushirikiana na Wananchi Wote Wa Rika zote Kampeni ya Kukomesha Vitendo/ Matukio ya Ukatili Dhidi ya Jinsia , Wanawake, Watoto na Wazee Nchini itakayokwenda kwa Jina la SHUJAA WA MAENDELEO NA USTAWI WA JAMII TANZANIA (SMAUJATA).
Kauli Mbiu Ikiwa ni;
Kataa Ukatili, Wewe ni Shujaa .
MALENGO MAKUU YA SMAUJATA
1. Kushirikisha Jamii katika kuainisha fursa na changamoto
zinazoikabili ili kulijiletea Maendeleo
2. Kuelimisha Jamii kuondokana na Fikra, Imani, Mila, Desturi
na Tamaduni Zinazokinzana na Maendeleo
3. Kushirikisha Jamii katika Kuiunganisha na Kuiwezesha katika Mchakato wa Maendeleo ili
kuinua ustawi wake.
4. Kuratibu Utekelezaji na Uzingatiaji wa Masuala ya Jinsia
Katika Programu na Mipango ya Maendeleo Katika Sekta
Mbalimbali
5. Kuwezesha Jamii Kutumia Fursa ya Sera za Kisekta na
Mikakati yake katika Kujiletea Maendeleo.
6. Kutoa Elimu Kwa Jamii Kupitia | Semina | sanaa | Warsha | Makongamano | Vyombo vya Habari, | Matembezi ya Amani | Vipeperushi Kuhusu Haki | usawa | Fursa | na Sera mbadala kwa Maendeleo Endelevu na Kuiwezesha Jamii Kutekeleza Haki na Malezi ya Mtoto
7. Kuibua, Kuendeleza na Kukuza Vipaji Mbalimbali katika Ujuzi, Utaalamu na Ubunifu ili Kujenga Kizazi chenye Uwezo wa Kujitegemea.
8. Kushirikiana na Serikali, Wananchi, Wadau mbalimbali Kutoka Ndani na nje ya Nchi katika Shughuli za Utoaji wa Elimu na Fursa za Maendeleo.
9. Kupokea Mbinu wezeshi, Maoni na Mawazo Mapya kutoka Makundi mbalimbali ya Wadau na Kuishauri Jamii na Serikali katika Kuboresha na Kufanikisha Vipaumbele vya Ustawi na Maendeleo ya Jamii.
10. Kufanya Shughuli zingine Zozote zinazohusu Maendeleo na Ustawi wa Jamii.
Kwa mawasiliano
NDG. SOSPETER MOSEWE BULUGU
SIMU: 0753725034
[email protected]
MWENYEKITI WA SMAUJATA TAIFA
(KAMPENI YA KITAIFA KUPINGA UKATILI DHIDI YA WATOTO, JINSIA NA MAKUNDI MAALUM)
KATAA UKATILI , WEWE NI SHUJAA
Day | Members | Gain | % Gain |
---|---|---|---|
May 20, 2024 | 389 | +1 | +0.3% |
March 01, 2024 | 388 | +2 | +0.6% |
January 11, 2024 | 386 | 0 | 0.0% |
November 28, 2023 | 386 | +2 | +0.6% |
October 24, 2023 | 384 | 0 | 0.0% |
September 24, 2023 | 384 | 0 | 0.0% |
August 26, 2023 | 384 | 0 | 0.0% |
July 23, 2023 | 384 | -1 | -0.3% |
June 28, 2023 | 385 | +77 | +25.0% |