VIJANA WAKATOLIKI TZ on Clubhouse

VIJANA WAKATOLIKI TZ Clubhouse
3.3k Members
Updated: Jun 23, 2022

Description

JUMUIYA YA MTAKATIFU PAPA YOHANE PAULO II ONLINE 📶

JUMUIYA YA SALA YA KIKATOLIKI TANGU JULY 27 2021📍🗓

✝️

RATIBA YA SALA ZA JUMUIYA

🙏 Rozari ya Moyo Mtakatifu wa Yesu - Kila Siku Saa 11:15 Alfjiri (05:15 am)

🙏Sala ya Malaika wa Bwana - Saa 11:55 Asubuhi(05:55am), Saa 05:55 Asubuhi(11:55am) na Saa 11:55 Jioni(17:55pm)

🙏Sala za Asubuhi - Kila Siku saa 12:00 Asubuhi (06:00am)

🙏Rozari ya Huruma ya Mungu - Kila Siku Saa 08:45 Mchana( 14:45pm).

🙏Rozari Takatifu ya Fatima | Tafakari ya Injili | Maisha ya Watakatifu - Kila Siku Saa 02:20 Usiku (20:20pm)

🙏Ibada ya njia ya Msalaba - Kila Ijumaa Saa 08:45 Mchana ( 14:45pm)

🙏Rozari ya Mateso 7 ya Bikira Maria - Kila Jumanne Saa 02:20 Usiku (20:20pm)

✝️

SALA KWA MTAKATIFU YOHANE PAULO WA II

Ee, Mtakatifu Yohane Paulo, kutoka kwenye dirisha la mbinguni, utujalie baraka yako! Libariki Kanisa ulilolipenda na kulitumikia na kuliongoza, ukiliongoza kwa ujasiri katika njia za ulimwengu ili kumleta Yesu kwa kila mtu na kila mtu kwa Yesu. Wabariki vijana, ambao walikuwa shauku yako kubwa. Wasaidie kuota tena, wasaidie kutazama juu tena ili kupata nuru inayoangazia njia ya maisha hapa duniani.

Ubariki kila familia! Ulionya kuhusu shambulio la Shetani dhidi ya cheche hii ya kimungu yenye thamani na ya lazima ambayo Mungu aliwasha duniani. Mtakatifu Yohane Paulo, kwa maombi yako, ulinde familia na kila maisha yanayochanua kutoka kwenye familia.

Ombea ulimwengu wote, ambao bado unatawaliwa na mivutano, vita na ukosefu wa haki. Ulipambana na vita kwa kukaribisha mazungumzo na kupanda mbegu za upendo: utuombee ili tuwe wapandaji wa amani bila kuchoka.

Ee Mtakatifu Yohane Paulo, kutoka kwenye dirisha la mbinguni, tunapokuona karibu na Mariamu, tuma baraka za Mungu juu yetu sote. Amina.

✝️

SALA YA SINODI

Tunasimama mbele yako Ewe Roho Mtakatifu, Tunapokusanyika pamoja kwa Jina lako.

Wewe pekee unayetuongoza, Weka maskani yako ndani ya nyoyo zetu; Utufundishe njia ya kupita na jinsi ya kuenenda.

Sisi ni dhaifu na wenye dhambi;
Usiruhusu tuendelee kuchochea machafuko.
Usiruhusu ujinga utuongoze kwenye nijia mbaya, wala utepetevu usiathiri matendo yetu.

Utuwezeshe ndani Yako tuwe na umoja
ili tuweze kusafiri pamoja hadi uzima wa milele, wala tusipotee mbali kutoka njia ya kweli na iliyo sahihi.

Tunaomba hayo yote, Kwako Wewe ufanyae kazi kila mahali na kila wakati,
katika ushirika wa Baba na Mwana, milele na milele, Amina.

Rules

Karibu Sana

Tumsifu Yesu Kristo(Milele Amina). Tupo hapa kwa ajili ya kusali na kuimarishana kiroho. Jambo lolote lisilo husu Ukatoliki halitavumiliwa.

Tuheshimu kila mtu katika Club

Kila mmoja ana nafasi sawa na mwengine! Hatavumiliwa mtu kwa njia yoyote ile ambayo ataonyesha kuvunja heshima na utu wa mwengine. Lugha za matusi haziruhusiwi.

Last 30 Records

Day Members Gain % Gain
June 16, 2022 3,300 +100 +3.2%
June 09, 2022 3,200 +3,200 +320,000.0%
May 21, 2022 0 -3,100 -100.0%
May 07, 2022 3,100 +100 +3.4%
April 23, 2022 3,000 +100 +3.5%
April 09, 2022 2,900 +100 +3.6%
April 03, 2022 2,800 +100 +3.8%
March 18, 2022 2,700 +100 +3.9%
March 11, 2022 2,600 +614 +31.0%
November 23, 2021 1,986 +5 +0.3%
November 22, 2021 1,981 +15 +0.8%
November 19, 2021 1,966 +25 +1.3%
November 16, 2021 1,941 +3 +0.2%
November 15, 2021 1,938 +7 +0.4%
November 14, 2021 1,931 +8 +0.5%
November 13, 2021 1,923 +13 +0.7%
November 12, 2021 1,910 +9 +0.5%
November 11, 2021 1,901 +3 +0.2%
November 10, 2021 1,898 +12 +0.7%
November 08, 2021 1,886 +19 +1.1%
November 06, 2021 1,867 +4 +0.3%
November 05, 2021 1,863 +7 +0.4%
November 04, 2021 1,856 +4 +0.3%
November 03, 2021 1,852 +38 +2.1%
November 01, 2021 1,814 +9 +0.5%
October 31, 2021 1,805 +8 +0.5%
October 30, 2021 1,797 +13 +0.8%

Charts

Some Club Members

More Clubs